Jinsi ya kuuza bidhaa Facebook tsh 100,000 kwa siku

Katika kipindi chetu cha leo tunakwenda kujifunza jinsi ya kuuza bidhaa zako katika mtandao wa facebook. Tunafahamu kwamba hivi sasa watu wengi wanatumia mitandao ya kijamii na wanatumia muda wao mwingi sana katika facebook page na facebook kwa ujumla.

Jinsi ya kuuza bidhaa Facebook


Kuuza bidhaa zako katika mtandao wa facebook ni uchaguzi sahihi sana kwani unakwenda kupata wateja wengi wanaotumia mitandao huu.

Kutangaza katika facebook kuna njia Tatu kuu,

Njia ya kwanza: kutumia facebook group:

Hii inahusisha kufungua facebook group na kuanza kutangaza biashara zako ndani ya group hilo. Kadri muda unavyozidi kwenda watu wataendelea kujiunga katika group lako na hivyo ndivyo utaendelea kuuza bidhaa zako. 

Uzuri wa facebook group watu wanaendelea kujiunga kadri siku zinavyozidi kwenda. 

Hivyo utaendelea kupata wateja wapya kadri muda unavyozidi kuongezeka. Kupata wateja, inakuhitaji uweze kutoa mafunzo katika group lako na mwisho wa siku uweze kuweka matangazo yako ya biashara ili watu wakuamini na waweze kununua bidhaa zako.

Njia hii ni njia inayotumiwa na watu wengi sana kutangaza bidhaa zao kwenye facebook.

Njia namba mbili:  kutumia facebook page:

Hii inahusisha kufungua Facebook page na kuanza kufanya matangazo ya biashara yako katika page hiyo. Katika facebook group kila mwanachama au mwana kikundi yeyote  anaweza kutoa maoni, kuposti na kutoa comments. 

Lakini katika facebook page wewe pekee ndio unaweza kuweka posti kwenye facebook page tu, wengine watalaiki na kucomment kitu ulichoweka wewe tu. 

Njia hii ni njia nzuri sana na inawashauriwa zaidi kwani watu watakaojiunga katika page yako wataendelea kuona matangazo yako tu,  peke yako kwani wewe ndio mwenye uwezo wa kuposti katika page. 

Kuuza zaidi bidhaa zako inakuhitaji uweke picha nzuri na maneno mazuri ambayo yatamvuta mteja kuweza kuangalia bidhaa zako na kununua.

Maneno ni lazima yawe mafupi, yanayoeleweka na yanayomshawishi mteja kuweza kununua bidhaa zako. Vivyo hivyo picha unazotumia ziwe na rangi nzuri zinazoonyesha bidhaa na zinazoweza kuonyesha jinsi gani bidhaa inavyoweza kuwa muhimu kwa mteja.

Kwa kufanya hivi utaweza kupata wateja wengi sana wanaojiunga katika page yako. lakini pia wateja wanaweza kununua bidhaa zako kiurahisi zaidi.

Njia ya tatu ni kwa kutumia facebook ad:

Facebook ad haya ni matangazo ya facebook, matangazo haya yanalipiwa hela kadhaa ili kuweza kuwafikia wateja wengi kwa muda mfupi. Yaani unaweka tangazo kuhusu bidhaa zako na facebook  wanakusaidia kufikisha tangazo lako kwa watu 3000 au watu 5,000 kwa tsh 3000 ndani ya siku moja.

Hii ndio inaitwa facebook ads.

Njia hii ni maarufu sana kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwani unaweza kupata wateja kiurahisi isivyo kawaida.

Kwa kutumia facebook ads unaweza kuchagua jinsia gani ya watu waone tangazo lako, umri gani wa watu waone tangazo lako au watu wanaopenda mambo fulani ndio waone tangazo. Kwa kufanya hivi unaweza kupata wateja wako kiurahisi.

Kama hufahamu jinsi ya kutengeneza facebook page na kufanya matangazo ya facebook, tunatoa huduma hizi kwa bei rahisi kabisa. 

Wasiliana nasi kuweza kupata huduma hizi za facebook page facebook ya biashara, youtube channel na huduma zote zinahusiana na mtandaoni. 

Tunatoa huduma hizi kwa bei rahisi kabisa mahalo popote ulipo. Lengo ni kukuza biashara zetu na kuwa za kisasa.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutangaza bidhaa zako katika mtandao wa facebook:

1. Lazima utengeneze facebook page ili kutangaza bidhaa zako katika mtandao wa facebook.

Ni vigumu sana kutangaza bidhaa zako katika profile yako ya facebook. 

Watu wengi wanaotaka kununua bidhaa ya kutoa kwako hawatakuamini kwani profile yako haitakuwa na maelezo ya kutosha kama ukitengeneza facebook page au facebook group.

Hivyo inashauriwa ili waweze kuuza bidhaa zao kiurahisi huku ukiaminiwa na wateja wako ni heri kutengeneza facebook page au facebook group yako.

Wasiliana nasi kupata huduma ya kutengeneza Facebook page na jinsi ya kufanya matangazo:


Phone: 🚀 0629965180

Email: 🚀 tuma email


 2. Tumia picha nzuri

Kuhakikisha unapata wateja wengi katika mtandao wa facebook ni heri kutumia picha nzuri. 

Picha ambazo zinavuta wateja kwa asilimia 100. Kumbuka kwamba mchanganyiko mzuri wa rangi unapendwa sana na wateja, hivyo hakikisha picha zako zinamchanganyiko mzuri wa rangi. Kumbuka kuweka picha ya bidhaa yako unayeuza katika picha zako kwani hali hii itawavutia wateja wengi kuinunua bidhaa zako.

3. Tumia maneno mafupi yenye ushawishi.

Ili kuweza kuwavutia hateja wengi kununua hakikisha umetumia maneno mafupi yasiozidi maneno 100 ili kuweza kumlahisishia msomaji kusoma kwa muda mfupi na kuelewa kazi ya bidhaa yako.

Kwa kufanya hivi wateja wengi watasoma maneno mafupi na yenye maana na yatawashawishi kwenda kuiangalia bidhaa yako na ikiwezekana kuinunua kabisa.


Ni muhimu kutoa maelezo jinsi gani bidhaa hiyo inakwenda kumsaidia mteja wako kutatua tatizo lake, kwa kufanya hivyo bidhaa yako itawahi kununuliwa kwani watajua kazi kuu ya bidhaa yako ni nini.


Hakikisha umeweka kazi moja au mbili muhimu ya bidhaa zako ili kuweza kumlahisishia msomaji kuelewa kiurahisi kazi ya bidhaa yako.

Na hivyo ndivyo jinsi ya kuuza bidhaa zako katika facebook, kwa kufuata muongozo huu, unaweza kufanikisha kuuza bidhaa zako kwa wateja wengi sana na kufanikiwa kutengeneza hela nyingi katika mtandao wa facebook.

Hitimisho

Kuuza bidhaa katika mtandao wa facebook ni rahisi na kuna faida nyingi sana katika biashara yako. Facebook Kusaidia kuwafikia wateja wengi sana isivyo kawaida. 

Mtandao wa facebook unaweza kusaidia kukutana na wafanyabiashara wenzako wanaofanya biashara sawa na wewe na kuweza kubadilishana mawazo kuhusiana a mbinu mbalimbali za kuweza kuuza biashara yenu.

Unahitaji facebook page na facebook group ili kuanza kutangaza bidhaa zako katika mtandao wa facebook. 

Kupata facebook page na facebook group, wasiliana nasi tutakusaidia kufanya kazi hii kwa gharama nafuu na pia tunatoa maelezo na mafunzo ya jinsi gani ya kuweza kutengeneza matangazo ya facebook ili kuwafikia wateja wengi na kuuza bidhaa zako zaidi.


asante na karibu 🚀

0 Comments