Biashara ni nini?
Ni kitendo Cha kutengeneza bidhaa au kununua bidhaa na kuuza kwa lengo la kupata faida. Mfano wa biashara ni kununua mayai na kuuza, kununua kuku na kuuza au kutengeneza sabuni na kuuza.
Kuna aina za biashara nyingi, kwa kuzingatia sifa mbali mbali. Sifa hizo zinaweza kua Uzalishaji, Faida, Aina ya bidhaa, watumiaji, uwekezaji na muda.
Aina za biashara:
1. Aina za biashara Kwa kuzingatia Uzalishaji:
Kuna aina mbili za biashara ambazo ni:
(a) Biashara ya kutengeneza bidhaa mwenyewe
Hii ni biashara ambayo bidhaa unazalisha mwenyewe. Mfano watu wanaofanya biashara ya mikate, sabuni, ice cream, vitumbua, mandazi na chai. Hizi ni biashara ambayo bidhaa unazalisha mwenyewe kutoka kwenye vitu mbali mbali. Mara nyingi saana biashara hii inafaida kubwa sana kwa wewe ndio mzalishaji, Bei yeyote inakulipa.
(b) Biashara ya kununua bidhaa
Biashara ya kununua na kuuza bidhaa ni aina ya pili ya Biashara. Hii inahusisha kutafuta maduka yanayouza bidhaa kwa Bei ya chini na kuuza kwa Bei ya juu. Ukipata chimbo zuri, hii pia ni biashara nzuri sana.
Unahitaji kutafuta maduka yanayouza bidhaa kwa Bei nafuu zaidi kulinganisha na soko lako, Ili kupata faida nzuri.
Unaweza hata kujifunza kuagiza bidhaa kutoka China.
2. Aina za biashara kwa kuzingatia Faida
Kuna aina mbili za biashara ambazo ni:
(a) Biashara zenye Faida endelevu
Hizi ni biashara ambazo zinatoa Faida zinazoendelea. Yaani ukianza kupata pesa, inakua moja kwa moja . Biashara hizi zinahitaji uwekezaji wa muda na pesa Ili zianze kufanya kazi. Kwa mfano biashara za mtandaoni, ni moja biashara ambayo Zina Faida endelevu. Mfano watu wenye blog, YouTube channel, Duka la mtandaoni wanapata Faida endelevu. Biashara hizi zikianza kuingiza pesa, inakua endelevu.
Kama unahitaji YouTube channel, Blog na Duka la mtandaoni, tutakusaidia kufungua. Wasiliana nasi
Tazama huduma zetu 👈
(b) Biashara zenye Faida mara moja tu.
Hizi ni biashara ambazo unapata Faida mara moja tu ukiuza bidhaa Yako tu. Kwa mfano biashara ya nguo, utapata Faida pale unapouza nguo basi na hakuna Faida tena baada ya kuuza nguo.
Biashara zenye Faida mara moja tu sio nzuri kwa watu wenye mtaji mdogo, kwani unaweza kupata hasara ukikosa umakini katika biashara Yako.
3. Aina za biashara Kwa kuzingatia uwekezaji
Kuna aina tatu za biashara.
(a) Biashara ambazo hazihitaji mtaji.
Hizi ni biashara ambazo unaweza kuanza hata kama hauna mtaji wowote. Mfano wa biashara hivi ni Udalali wa nyumba, viwanja na vyumba. Biashara hizi unaweza kuanza kuwasaidia watu kununua, kuuza na kupata vyumba vya kupanga.
Pia Biashara za mtandaoni kwa mfano affiliate marketing, freelance writing na YouTube channel unaweza kuanza bila hata mtaji wowote.
(b) Biashara zinazohitaji mtaji endelevu
Hizi ni aina za biashara ambazo zinahitaji mtaji endelevu, yaani utanunua bidhaa na kuuza Kila mara. Mfano wa biashara hizi ni biashara ya Duka ambayo inahitaji kununua bidhaa Kila siku Ili uuze. Aina hii ya Biashara ni marufu sana katika nchi za Africa mashariki.
(c) Biashara ambazo zinahitaji mtaji mara moja tu.
Hizi ni aina za biashara ambazo unawekeza mara moja tu na kuanza kupata faida endelevu. Yaani ukimaliza kutengeneza biashara Yako, tayari huitaji kuwekeza pesa tena, Bali unakula Faida tu.
Mfano wa biashara hii ni Ununuaji wa hisa za kampuni, saluni za aina zote, kujenga nyumba za kupangisha na kufungua kalakana ya magari. Biashara hii ni nzuri saana kwa watu wasio na pesa za kutosha au wenye mtaji mdogo. Ni rahisi kupata pesa kwa kufungua biashara hii, kwani utapata Faida tu pasipo na kuwekeza pesa Kila siku.
4. Aina za biashara Kwa kuzingatia muda
(a) Kuna biashara za msimu
Hizi ni aina ya biashara ambazo zinakuja katika vipindi Fulani. Kwa mfano biashara ya kuuza miti ya krismasi na kuuza mbolea wakati wa mvua. Hizi ni biashara za msimu ambapo utauza zaidi msimu unapofika. Miti ya krismasi inatoka zaidi muda krismasi na mbole inauzwa muda wa masika.
Biashara hizi sio nzuri kwa utapata Faida nzuri kwa msimu. Ni heri kuchagua biashara ambazo unapata Faida muda wote.
(b) Biashara zisizo za msimu
Hizi ni aina za biashara ambazo zinahitajika muda wote. Biashara za aina hii zinatakiwa muda waote kwenye soko. Biashara ya vyakula ni moja kati ya biashara zisizo za msimu kwani chakula kinahitajika muda wote. Biashara za aina hii, zinafaida. Biashara hizi zinafaida sana kwani Zina wateja muda wote.
Kuna aina nyingi za biashara kutokana na sifa ulio zingatia wewe. Hivyo ni vyema kuchagua biashara kwa kuzingatia muda, uwekezaji, Faida na Uzalishaji.
Biashara ambazo hazihitaji mtaji ni nzuri kwa kuanza na kujaribu soko. Pia aina ya biashara ambazo zina mtaji endelevu ni nzuri saana kwani zinaweza kukusaidia kupata pesa nyingi.
Nyongeza:
ACHA kuuza biashara Yako kizamani, ni wakati wa kuweka biashara Yako mtandaoni.
Sisi Biashara plus+ tunatoa huduma ya kutengeneza Duka la mtandaoni, blog, YouTube channel, Facebook page na Duka la Whatsapp. Vyote hivi ni muhimu katika kukuza biashara Yako na kiwafikia wateja wengi Zaidi.
0 Comments